TIMU ya soka ya Yanga leo inatarajiwa
kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan
mjini hapa kutupa karata yake ya kwanza dhidi
ya Taifa Jang’ombe katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi iliyoanza jana visiwani
hapa.
Mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na
upinzani mkali utachezwa saa mbili usiku
baada ya ule wa Azam na KCCA ya Uganda
utakaochezwa saa 11 jioni. Mbali na mechi ya
Azam na KCCA pia kutakuwa na mechi ya
KMKM na Mtende itakayoanza saa tisa alasiri.
Katika mchezo wa mapema jana, JKU ilianza
vyema michuano hiyo kwa ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Mafunzo. Mabao ya JKY
yaliwekwa kimiani na Amour Omar katika
dakika ya saba na Isihaka Othman aliyefunga
dakika ya 27.
Katika hatua nyingine ratiba ya michuano hiyo
imelazimika kupanguliwa baada ya Villa SC ya
Uganda kujitoa. Awali timu hiyo ilitoa taarifa ya
kuja kushiriki na ilipangwa mechi ya kwanza
icheze na Yanga leo lakini imejitoa dakika za
mwisho.
Hivyo nafasi ya Villa sasa inachukuliwa Taifa
ya Jang’ombe katika kundi A ambalo
linaundwa na timu za Yanga, Polisi na Shaba.
Akizungumzia suala hilo jana Katibu wa Kamati
ya Michuano hiyo Khamis Said alisema
walipokea taarifa kutoka kwa Chama cha soka
Zanzibar (ZFA ambao ndio wanaotoa mialiko
na mawasiliano kwa timu mbali kuwa Villa
haitoshiriki.
Alisema kuwa sababu halisi ya timu hiyo
kubadilisha maamuzi yao mpaka sasa
hawajajua lakini inaonekana kuwa kwao
itakuwa ni vigumu kushiriki mashindano hayo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni