WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano
ya Ligi ya Mabingwa Azam wanatarajia
kucheza mechi ya kujipima nguvu na miamba
ya soka Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Azam imepangwa kuanza na El- Merreikh ya
Sudan katika mechi ya awali ya michuano ya
Ligi ya Mabingwa Februari mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili msemaji wa Azam
Jaffar Iddi alisema kikosi cha timu hiyo
kinatarajiwa kuondoka nchini kati ya Januari
28 na Februari 3 kuelekea Lubumbashi.
“Lubumbashi tutacheza mechi tatu za kirafiki
na TP Mazembe, Zesco ya Zambia na Don
Bosco.
Mwaka jana Azam ilishiriki michuano ya
Kombe la Shirikisho lakini haikufika mbali
baada ya kutolewa na Ferroviario de Nampula
katika hatua za awali. Azam kwa sasa iko
nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na
pointi 14 sawa na Yanga iliyo nafasi ya tatu.
Timu hiyo iliondoka Dar es Salaam jana
asubuhi kuelekea Zanzibar kwenye michuano
ya Kombe la Mapinduzi ambapo itacheza
mechi yake ya kwanza leo dhidi ya mabingwa
watetezi KCCA ya Uganda.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni