KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Yanga, Hans
Van de Pluijm amesema amefikia matarajio
yake juu ya kiwango kilichooneshwa juzi na
wachezaji wake kwenye mechi ya Kombe la
Mapinduzi dhidi ya timu ya Taifa ya
Jang’ombe.
Katika mechi hiyo ya kwanza kwa Yanga
kwenye michuano ya mwaka huu, iliibuka na
ushindi mnono wa mabao 4-0, matokeo
ambayo yamemfanya Pluijm kufunguka kuwa
hiyo ndiyo Yanga aliyoitarajia.
Katika mchezo huo, Yanga ambayo ilishuka
dimbani na mziki kamili, wachezaji wake
walionesha kiwango cha ubora ambacho wengi
wa mashabiki waliofika uwanjani hapo
walionekana kuridhika nacho.
Licha ya kucheza na timu ya Daraja la Pili
Taifa, lakini Yanga haikufanya ajizi katika
mchezo huo na kuonesha kucheza kwa
matumaini makubwa ya kutaka kushinda
pasipo na kuweka dharau yoyote kwa timu
hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
mchezo huo, kocha Pluijm alisema ameridhika
na kiwango hicho na kasoro ndogo ndogo
zilizojitokeza atazifanyia kazi.
“Nafikiria mashabiki wamefurahia mchezo,
wachezaji wangu wamecheza katika kiwango
kilicho bora na hivi ndivyo nilivyotarajia, kuna
baadhi ya kasoro ambazo zimejitokeza katika
mchezo huu lakini nitazifanyia kazi,” alisema.
Alisema kazi inayofuata hivi sasa ni kujipanga
kwa ajili ya mechi zinazofuata. Yanga katika
mchezo huo mabao yake yaliwekwa kimiani na
Simon Msuva aliyefunga mabao matatu na
moja likifungwa na Kpah Sherman.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni