TANZANIA
imezidi
kung’ara
katika
mchezo
wa tenisi
baada ya
jana
wachezaji
wake
wawili
kutinga
fainali
katika
michuano
ya Afrika
Mashariki
inayoendelea kwenye uwanja wa Gymkhana,
Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Deogratias Ernest na
Georgina Kemmy ambao walifanya vizuri
kwenye mchezo wa nusu fainali na
kuwashinda wapinzani wao.
Ernest aling’ara na kutinga fainali baada ya
kumshinda mpinzani wake Mtanzania Kanuti
Omar kwa seti mbili na kupoteza mchezo
mmoja.
Katika robo ya kwanza, Ernest alifungwa na
Kanuti seti 7-6, wakati Ernest alishinda
michezo miwili kwa seti 6-1, 6-1 na
kufanikiwa kuingia fainali ya vijana chini ya
umri wa miaka 16.
Aidha, Kemmy alitinga fainali baada ya
kumfunga Mrwanda Yabela Omurunga kwa
seti 6-1, 6-2. Wachezaji wengine waliofanya
vizuri na kuingia hatua ya nusu fainali ni
Emmanuel Mallya aliyeshinda michezo miwili
na kupoteza mmoja dhidi ya Tabres Kisime.
Alipoteza mchezo wa kwanza seti 6-2,
akashinda seti 6-3, 6-2 na kusonga mbele.
Wachezaji wengine ambao mwaka jana
waling’ara na kushindwa kufanya vizuri
mwaka huu katika mchezo wa robo fainali ni
Frank Menard aliyefungwa seti 7-5, 7-5 dhidi
ya mpinzani wake Rajab Mtamba. Pia, Omar
Sulle alishindwa kung’ara baada ya kufungwa
na Muethiopia Yadsir Kibade kwa seti 6-4,
6-3.
Kwa mujibu wa Kocha Majaliwa, Tanzania
imefanya vizuri kiasi kwani upinzani umekuwa
mkali mwaka huu ukilinganisha na mwaka
jana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni