MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki,
Shyrose Bhanji jana alifungua mashindano ya
Netiboli Taifa na kuahidi kutoa zawadi kwa
washindi watatu kwa kiasi cha Sh milioni 2.2
kwa ajili ya kuwahamasisha wachezaji
kucheza kiushindani katika michuano hiyo.
Mashindano hayo yatakayomalizika rasmi
Januari 13, mwaka huu yameshirikisha timu
kutoka Dodoma, Tabora, Arusha, Ilala,
Kinondoni, Temeke, Pwani na Mjini Magharibi
huku nyingine zikishindwa kufika kutokana na
sababu mbalimbali.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano
hayo, Bhanji alisema timu itakayofanya vizuri
ya kwanza itaondoka na Sh milioni moja, ya pili
Sh 700,000 na wa tatu Sh 500,000.
“Mikoa iliyofika imeonesha ari kubwa ya
mchezo huu, mimi nawaahidi kuwa timu
itakayofanya vizuri itapata zawadi,” alisema.
Alisema kuna haja kubwa kwa Kampuni na
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kuchukulia mchezo huo kama mpira
wa miguu na kuungwa mkono.
Bhanji pia, aliahidi kushirikiana na Chama cha
Netiboli Tanzania (CHANETA) katika
kushirikisha wadau wa michezo umuhimu wa
mchezo huo kwa ajili ya kuwavutia kuupenda
na kuusaidia.
Alisema ili mchezo huo uwe mzuri kuanzishwe
programu maalumu za Shule za Msingi
ambazo watoto watakuwa wakielimishwa
umuhimu wa mchezo huo, na hatimaye wakue
huku wakiwa wanaupenda.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chaneta
Anna Kibira alisema ukosefu wa fedha
wanaokabiliwa nao na ushirikiano kutokana na
vyama vya mikoani ndio ambao umesababisha
ushiriki wa timu za mikoani kuwa chache.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni