0

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Nassib
Abdul ‘Diamond Plutnamz’ anatarajiwa
kuburudisha kwenye sherehe za utoaji wa tuzo
za wanamichezo bora zinazoandaliwa na
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zitakazofanyika
Nigeria, Januari 8 mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba za shoo alizoweka
kwenye mtandao wake Diamond, baada ya
kufanya shoo kubwa Kigali, Rwanda inayofuata
ni hiyo ya tuzo za Glow-CAF.
“Nawashukuru mashabiki wa Rwanda kwa
kuniunga mkono katika shoo kubwa katika
sherehe za kuukaribisha mwaka, nawapenda
wote, sasa najipanga kuelekea Nigeria,”
alisema Diamond kwenye mtandao.
Diamond, ambaye alipata mafanikio makubwa
mwaka jana kwa kutwaa tuzo nyingi za
kimataifa, atafanya shoo hiyo kubwa kisha
atarudi Dar es Salaam kufanya nyingine kabla
ya kwenda Zanzibar na Mwanza aliko alikuwa
kwa ajili ya burudani.
Kwa mujibu wa mtandao wa glowworld,
wasanii wengine wa Afrika walioalikwa
kutumbuiza ni Hugh Masekela kutoka Afrika
Kusini, Flavor wa Nigeria, Fally Ipupa wa
Congo DRC, Hakim kutoa Misri, Kikundi cha
kwaya cha Pan African kutoka Soweto Afrika
Kusini na kundi la P-Square.
Katika tuzo hizo ambazo huandaliwa kila
mwaka zaidi ya wachezaji 40 wa Afrika
wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi zao,
na wale wanaocheza ndani ya Afrika
wanawania.
Tuzo zinazowaniwa ni mchezaji bora wa Afrika
wa mwaka anayecheza nje, pia anayecheza
ndani ya Afrika, timu bora ya taifa ya mwaka,
klabu bora ya mwaka na kocha bora wa
mwaka.
Nyingine ni timu bora ya taifa ya wanawake,
mwanasoka bora wa kike wa mwaka, chipukizi
bora, mwamuzi bora, gwiji bora na mchezaji
wa jumla.
Wachezaji mbalimbali ambao waliwahi
kushinda tuzo hizo ni Samuel Eto’o wa
Cameroon mwaka 2005 na 2010, Didier Drogba
wa Ivory Coast mwaka 2006 na 2009, Frederic
Kanoute wa Mali mwaka 2007, Emmanuel
Adebayor wa Togo 2008, Yaya Toure wa Ivory
Coast mwaka 2011, 2012 na 2013, anapewa
nafasi kubwa pia mwaka huu.

Chapisha Maoni

 
Top