KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Jang’ombe,
Othman Barik, amesema kuwa sababu kubwa
iliyowafanya wafungwe na Yanga ni kutokana
na wachezaji kuwa na hofu kubwa ya mechi,
jambo ambalo liliwagharimu.
Hayo aliyaeleza juzi baada ya kumalizika kwa
mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi ambapo
timu hiyo ilifungwa mabao 4-0.
Alisema wachezaji wake mwanzo walikuwa
wameukamia mchezo huo lakini baada ya
kufika uwanjani walitawaliwa na hofu na hivyo
kufungwa.
Aidha alisema, pamoja na hofu lakini viungo
wake hawakucheza vizuri huku ugeni wa
baadhi ya wachezaji wake nao ukichangia.
Sambamba na hilo kocha huyo alisema kuwa
huwezi kuifananisha Yanga na timu yake
kutokana na timu hiyo kusheheni wachezaji
wengi wazoefu.
“Silaumu sana wachezaji wangu kwani Yanga
huwezi kuifananisha na timu yangu kuanzia
mwanzo hadi mwisho Yanga ni timu iliyojaa
wachezaji bora,” alisema.
Aidha alisema kuwa kufungwa kwa mchezo
huo hakujamfanya akate tamaa ya kusonga
mbele na badala yake anajipanga kurekebisha
makosa ili mchezo ujao washinde.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni