0

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga Simon
Msuva amesema kuwa juhudi binafsi na
ushirikiano walionao katika timu
umemwezesha kuibuka mchezaji bora wa
mchezo Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa ya
Jang’ombe juzi ambapo Yanga ilishinda mabao
4-0.
Msuva ambaye aliifungia mabao matatu kati ya
manne timu yake alichaguliwa mchezaji bora
wa mechi hiyo na jopo la Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar
(ZASWA).
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo
aliyokabidhiwa na mlezi wa ZASWA, Harouna
Ali Suleiman alisema kuwa amefurahia kupata
nafasi hiyo ambayo ilitokana na ushirikiano
mkubwa na wachezaji wenzake.
“Ni juhudi zangu binafsi lakini zimetokana sana
na ushirikiano uliooneshwa na wachezaji
wenzangu,” alisema.
Aidha, aliwataka wachezaji wenzake kuzidi
kumpa ushirikiano popote timu yao inapocheza
ili kuendelea kufanya vizuri.

Chapisha Maoni

 
Top