0

KOCHA wa Mbeya City, Juma Mwambusi
amezitaka timu ambazo wanatarajia kukutana
nazo kujiandaa kwa kipigo, kwani tayari
wamerudi kwenye kiwango chao cha msimu
uliopita.
Mwambusi alisema ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya Ndanda FC, umewaimarisha na
kuwarudisha kwenye ligi baada ya kuanza
vibaya msimu huu na kujikuta ikiwa na pointi
tano katika mechi saba ilizocheza msimu huu.
“Tupo vizuri kwa sasa baada ya kugundua
mapungufu yetu na kuyarekebisha mapema
kwa faida ya mashabiki wetu ambao kwa sasa
naamini wataifurahia timu yao kama
ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema
Mwambusi.
Mwambusi aliyekaribia kuiacha timu hiyo
iliyomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita
kutokana na kutofautiana na viongozi wa juu,
alisema mabadiliko aliyoyafanya kwenye kikosi
chake kwenye dirisha la usajili yatabadili
mwenendo wa timu hiyo na kufanya vizuri.
“Tunaweza kuwa mabingwa kwa sababu
pamoja na kuwepo nafasi ya 12, lakini tofauti
yetu na Mtibwa Sugar inayoongoza ligi ni pointi
nane, kwa hiyo tumerudi kivingine tukiwa na
lengo la kutaka ubungwa msimu huu,” alisema
Mwambusi.
Mbeya moja ya timu ambayo iliwavutia
mashabiki wengi wa soka nchini kutokana na
aina ya soka lake na ushindani ilioutoa kwa
timu kubwa za Simba, Yanga na Azam, lakini
msimu huu imejikuta ikiwa katika wakati
mgumu baada ya kufungwa mechi nne
mfululizo katika mechi saba za awali.

Chapisha Maoni

 
Top