0

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Simba na
timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Henry
Joseph amesema anajiona mwenye furaha
kuifunga timu yake ya zamani kwa sababu ili
muacha kwenye kikosi chake kwa majungu na
kusingizia kiwango chake kimekwisha.
Joseph aliyewahi kuwa nahodha wa Simba na
Taifa Stars ndiye mfungaji wa bao pekee la
Mtibwa Sugar, wakati timu hizo zilipokutana
kwenye mchezo wa Kundi C wa michuano ya
Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye
Uwanja wa Amani Zanzibar.
“Najisikia furaha kubwa kwa kuipa ushindi timu
yangu, lakini kuifunga Simba kwa sababu ni
timu ambayo niliichezea kwa mapenzi yangu
yote na mwisho wa siku ikaja kuniacha kwa
fitina za watu wakisema sina uwezo,” alisema
Joseph.
Kiungo huyo aliyejiunga na Mtibwa kwenye
dirisha dogo la usajili wa msimu huu akiwa
mchezaji huru, alisema ataendelea kujituma
kuhakikisha anaipa mafanikio, ikiwemo kutwaa
ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu timu
yake mpya anayoichezea kwa sasa.
“Tuna timu nzuri na ndiyo maana tunaongoza
ligi mbele ya Azam na Yanga ambazo zipo
vizuri kwa sasa na lengo letu ni kuhakikisha
tunacheza kwa kujituma ili tuweze kufanya
kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi
mwaka huu,” alisema Joseph.
Kabla ya kurudi Simba msimu uliopita, Joseph
alikuwa akicheza soka la kimataifa kwenye
klabu ya Kongsvinger IL, inayoshiriki ligi daraja
la kwanza nchini Norway na baada ya
kumaliza mkataba wake na timu hiyo alirudi
tena Simba na kudumu kwa msimu mmoja
kabla ya kutupiwa virago.

Chapisha Maoni

 
Top