KIUNGO mchezeshaji wa Yanga, Haruna
Niyonzima amesema kugombea namba katika
kikosi hicho ndio hufanya kuendelea kujituma
uwanjani ili kiwango chake kisishuke.
Akizungumza na gazeti hili, Niyonzima alisema
amekuwa akifanya juhudi katika kuhakikisha
timu yake inaondoka na pointi zote tatu katika
kila mchezo ingawa wakati mwingine hukutana
na ugumu katika kutimiza malengo.
Alisema ili kiwango chake kiwe bora na
kuendelea kuaminiwa na timu hiyo ataendelea
kucheza kwa kiwango cha hali ya juu na
kukisaidia kikosi hicho kufanya vyema.
“Ni kweli kwamba wakati mwingine namba
inaweza ikawa ni sababu ya sisi kujituma kwa
ajili ya kuendelea kubaki katika timu, lakini
tunapambana kuhakikisha kiwango
kinaimarika,”alisema.
Niyonzima alisema moja ya malengo yake ni
kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kufanya
vyema, akiamini pointi ndio muhimu kwao.
Alisema kwa kulitambua hilo ndio maana
wanapoingia uwanjani hucheza kwa kujituma
na kushambulia kupata ushindi wa mapema.
Katika msimu uliopita Niyonzima kiwango
chake kilionekana kushuka kutokana na
matatizo yaliyokuwa yakimkabili lakini sasa
mambo yanakwenda vizuri baada ya kucheza
kwa kujituma.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni