0

WATU wawili wamekufa mkoani Singida katika
matukio tofauti yaliyotokea hivi karibuni,
likiwemo la mwanamke mmoja kupigwa na
rungu na mumewe kutokana na kile
kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida,
Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio la
kwanza lililotokea kijiji cha Songambele, kata
ya Ndago wilayani Iramba Januari 11 mwaka
huu majira ya saa 1.00 asubuhi ni la mauaji ya
Maria Shila (57) yaliyofanywa na mumewe
Lucas Kitundu (47).
Akisimulia mkasa huo, Sedoyeka alisema
kuwa kabla ya tukio hilo wana ndoa hao
walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara
ambapo Kitundu alikuwa akimtuhumu mkewe
Maria kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao.
Alisema kuwa siku ya tukio, wanandoa hao
walionekana klabu ya pombe ya kienyeji
wakiwa wanalumbana na asubuhi ya siku
iliyofuata mwili wa Maria uligundulika ukiwa
umetelekezwa nje ya nyumba yao huku
pembeni mwake kukiwa na rungu lililojaa
damu.
“Aliyegundua mwili huo ni mdogo wa
marehemu ambaye alikuwa na miadi ya
kumpitia siku hiyo kwa ajili ya kwenda naye
kanisani,” alisema Kamanda Sedoyeka.
Kamanda Kamwela alisema kuwa uchunguzi
wa awali wa Polisi unaonesha kuwa Kitundu
alikuwa akiishi nyumbani kwa marehemu na
mara baada ya kufanya kitendo hicho
alichukua vitu vyake, zikiwemo nguo, na
kutoweka kusikojulikana ambapo hadi sasa
hajapatikana.
Katika tukio la pili lililotokea Januari 12 mwaka
huu huko katika kijiji cha Mguluwang’ombe
wilayani Manyoni, mtoto Laurent Buji (5)
alipoteza maisha akiwa njiani kupelekwa
hospitalini kwa matibabu baada ya kutumbukia
kwenye shimo la choo lililokuwa limejaa maji.

Chapisha Maoni

 
Top