0

Dar es Salaam. Wakati Halmashauri Kuu ya
Chama cha ACT-Tanzania ikikutana kujadili
agenda tatu, ikiwamo ya kuazimia kumvua
uongozi Mwenyekiti, Kadawi Limbu, Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa leo inawakutanisha
viongozi waandamizi wa chama hicho kusaka
suluhu ya mgogoro wao.
Chama hicho kwa siku za hivi karibuni
kimekuwa katika mvutano kati ya Limbu na
viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu, Samson
Mwigamba.
Viongozi wengine wanaosubiriwa na rungu la
kikao cha halmashauri kuu ni Naibu Katibu
Mkuu (Bara), Leopold Mahona na Mwenyekiti
wa Ngome ya Vijana, Grayson Nyakarungu.
Juzi gazeti hili lilimnukuu, Msaidizi wa Msajili
wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akisema:
“Mvutano huu hata sisi tunausikia, tumeamua
kuwaita Jumanne hii (leo) ili tuwasikilize wote
kwa pamoja.”
“Tumewaita siyo kwa lengo la kuendeleza
tofauti zao, bali kuzimaliza baada ya kusikiliza
kila upande.”
Akifungua kikao cha halmashauri kuu jana,
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Tanzania (Bara),
Shaban Mambo alisema:
“Mkutano huu ni halali kisheria, kikatiba na
kikanuni, hivyo nawasihi wajumbe msiwe na
hofu na mjadili kwa kujenga hoja na
unapokuwa huelewi usiogope kuuliza.”
Aliongeza: “Kila chama lazima kipite katika
matatizo na unapopita katika matatizo kama
haya ndiyo chanzo cha mafanikio na kukua kwa
demokrasia, hatutaogopa kusema ukweli na
kutenda haki ni jadi yetu.”
Akitaja ajenda za kikao hicho, Mwigamba
alisema ni kupokea na kujadili taarifa ya chama
kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na
Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Akifafanua ajenda hizo alisema, watapitisha
mapendekezo ya ratiba ya uchaguzi wa ndani
iliyopendekezwa na Kamati Kuu Januari 5,
mwaka huu kuanzia Januari 19 hadi Machi 28
mwaka huu.
Aidha, watajadili taarifa ya hali ya kisiasa ndani
ya chama, ikiwamo taarifa ya kamati maalumu
iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi ya Limbu
na wenzake.
Kuhusu akidi alisema kikao hicho kinapaswa
kuwa na wajumbe 88 na akidi yake ni asilimia
50, ambayo ni sawa na wajumbe 44 na
waliohudhuria walikuwa wajumbe 63 ambao
wamevuka idadi inayotakiwa.
Katika hatua nyingine, aliyewahi kuwa Katibu
Mkuu wa Tanzania Labour Party (TLP), Hamad
Tao amejiunga na ACT-Tanzania na kusema
ameamua kujiunga na chama hicho kutokana na
kukubali sera zake

Chapisha Maoni

 
Top