0

Simba SC jana ilitwaa ubingwa huo katika uwanja
wa Amani baada ya kuwafunga Mtibwa Sugar kwa
mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90
kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Simba SC walionekana kuwa na uwezo wa
kumaliza mchezo ndani ya dakika 90 lakini umahiri
wa kipa Said Mohamed na kupoteza umakini kwa
washambuliaji wa Simba SC kulipelekea dakika 90
kumalizika kwa bila kufungana.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar jana walitengeneza
nafasi mbili pekee ambazo nao walishindwa
kuzitumia na muda mwingi wakitumia katika kuzia
huku wakipiga mipira mirfu ambayo Ame Ally
alishindwa kuitendea haki.

Chapisha Maoni

 
Top