VIJANA 16,594 waliohudhuria mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wameajiriwa na
vyombo vya Ulinzi na Usalama kuanzia
mwaka 2011 hadi 2014.
Katika ajira hizo, 12,499 waliajiriwa na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi, 2,745 jeshi la Polisi, 1,107
jeshi la Magereza, 100 jeshi la Zimamoto na
143 Usalama wa Taifa.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Hussein Mwinyi aliliambia Bunge jana wakati
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rita
Kabati (CCM) aliyetaka kufahamu idadi ya
vijana walionufaika kwa kupitia JKT na lini
wafanyakazi walioko serikalini na wabunge
ambao hawajapitia JKT wataendelea na
utaratibu huo. Akijibu swali hilo, Mwinyi
alisema serikali haijaweka utaratibu kisheria
wa kuwataka watumishi wake kupitia mafunzo
ya Jeshi la Kujenga Taifa kama ilivyokuwa
hapo awali. Alisema sheria iliyopo ni kwa
wahitimu wa kidato cha sita kuhudhuria
mafunzo hayo, aidha wizara ipo tayari
kuendelea kutoa mafunzo ya jeshi la kujenga
taifa kwa wabunge vijana kadri itakavyopokea
orodha ya wabunge. Katika swali la nyongeza,
Kabati alihoji kwa nini vijana waliobaki
wasiajiriwe katika maeneo ya Bandari, kulinda
wanyamapori, Halmashauri na Jiji pamoja na
kwa nini vijana hao wasipewe mitaji na serikali
ili kujiajiri kutokana na mafunzo ya stadi za
kazi walizopata JKT. Akijibu swali hilo, Mwinyi
alisema ni vigumu kuajiri vijana wote waliotoka
JKT, lakini wamekuwa wakiajiliwa na Taasisi
nyingine kama bandari, Tanapa na halmashuri
mbalimbali na kuhusu mitaji ili wajiajiri alisema
atakaa na wizara zinazohusika na vijana kuona
jinsi ya kupata mitaji hiyo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni