Kwa mara kibao Vanessa Mdee na Jux
wamekanusha kuwa na uhusiano wa
kimapenzi licha ya kuonesha dalili
nyingi ya kuwa ni item
Lakini huenda mastaa hao wanataka
kuufanya uhusiano wao official kwa
mwaka 2015. Vee Money ametoa hint
kuhusu uwezekano wa wawili hao
kuwa pamoja kwenye picha aliyoweka
Instagram leo.
“A1 since Day 1,” ameandika Vanessa
kwenye picha hiyo ya black and white
inayoonesha wazi kuwa wapo kwenye
dimbwi la mahaba mazito.
Naye Jux amepost picha akiwa na Vee
na kuandika:
I know I’m late but better late than
never. Nataka kuwashukuru wote kwa
Upendo wenu mlionyesha Mwaka wa
2014, nawa ahidi burudani zaidi na
mziki mzuri zaidi this year and
hopefully through Gods grace in the
years to come. God bless your 2015. I
got to share mine with Miss Award
Winner #AfricanBoy #InGodITrust.”
Akijibu swali la kama ana uhusiano wa
kimahaba na muimbaji huyo wa
‘Nitasubiri’, Vanessa aliwahi
kujibu,”Unajua labda watu hawafahamu
tu lakini mie na Jux tumefahamiana
muda sana na ni mtu ambaye huwa
tunashauriana hasa mambo ya kazi
zetu.”
“Ni rafiki yangu wa muda sana sasa
hivi. Unajua watu wakikuona upo na
mtu karibu tu lazima watasema.
Mwanzo walisema Ommy Dimpoz
sababu ya ile nyimbo ya Me and You.
Mara wakasema Gosby kipindi kile
ilipotoka ile nyimbo ya Monefere.
Kwahiyo kwahiyo hata leo mfano
Nahareel asingekuwa na Aika basi
nahisi na yeye pia wangesema hivyo.
Ila sio hivyo wanavyofikiria. Jux ni
rafiki yangu tu,” Vee aliiambia Bongo5.
Naye Jux alikuwa na majibu yale yale
pindi swali hilo lilipokuwa likitupwa
kwake. “No ni mshikhaji wangu tu,
tunafanya naye kazi, kuna tabia
zinaendana, kama ninavyokuwa na
rafiki na Stamina, Mo Music ni
kawaida, sema unajua ni mwanamke
na ni njia toafuti ndio maana imekuwa
hivyo,” alisema Jux.
Hata hivyo alipoulizwa kama Vanessa
anafaa kuwa wife material Jux alijibu
Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke.
“Ni msichana mzuri, mwonekano wake
mzuri, she is smart, yeah she is a wife
material, yuko vizuri, lakini na mimi
tumeendana sana tabia zetu kama
washikaji. Sema nipo naye karibu na
kwa sababu mimi sionekanagi na
wasichana wengi ndio maana imekuwa
hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa
sasa hivi ni mapema, vyote anapanga
Mungu,” alisisitiza Jux.
Related Posts
MWANAMKE MMOJA AWAUWA WANAE NA KUWAZIKA NDANI
Hii Dunia sijui inaelekea wapi, na sijui mwisho wake ni nini... lakini nahisi nakosea kuilaumu Dunia[...]
Jan 26, 2015MSHINDI WA BIG BROTHER 2014 ANUNUA NYUMBA YAKIFAHALI
Ule usemi kuwa hakuna ‘baba/mama mwenye gari’ mjini bali kuna ‘baba/mama mwenye ny[...]
Jan 23, 2015WHY OBAMA'S INDIA REPUBLIC DAY VISIT IS SIGNIFICANT
The most significant aspect of the US President, Barack Obama's upcoming summit with the Indian Prim[...]
Jan 22, 2015MWANAUME MWENYE HIPS KUBWA KUWAZIDI KIM K,NICK MINAJ NA MASOGANGE
Micah ni mwanaume…lakini ana hips kama au zaidi ya mwanamke! Zile hips ambazo baadhi ya wadada[...]
Jan 20, 2015ZALI HAWEZI KUZAA NA DIAMOND MUME AFICHUA SILI NZITO
Oohoo! Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiche[...]
Jan 19, 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.