Hii Dunia sijui inaelekea wapi, na sijui mwisho
wake ni nini... lakini nahisi nakosea kuilaumu
Duniaila wanokaa katika hii Dunia ndio
wanafanya ionekane ya ajabu. Binaadamu
tumebadilika sana, na hatuna tofauti na
wanyama sasa hivi, kwani haiingii akilini mtu
kwa akili yako timamu kabisa ufikie uamuzi
kama alioufikia huyu mama.
Huko mkoani Tabora katika Kat ya Chemchem,
mama huyu ambaye jina lake halikuweza
kufahamika, aliwauwa watoto wake wawili na
kuwazika kabisa eti kwa vile alikimbiwa na
mume wake na yeye hana uwezo
wakuwatunza hivyo akaamua awauwe kisha
awazike ili abaki peke yake.
hii kweli ni akili ya kibinaadamu au ya kinya?
watanzania tunakwendda wapi?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni