Oohoo! Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro-
Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichekelea
kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan
‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kunasa mimba yake,
habari ya mjini huko Kampala, Uganda ni juu ya
aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, Ivan
Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari
hawezi kuzaa na Diamond.”
HABARI YA MJINI
Wikiendi iliyopita, vyombo vya habari na mitandao
nchini Uganda ambako kuna makazi mengine ya
Zari mbali na Afrika Kusini, kulipambwa na habari
hizo baada ya mwanaume huyo aliyezaa na
mwanamama huyo watoto watatu kuanika siri nzito
juu ya ishu hiyo.
‘Ubuyu’ huo ulidadavua kwamba, kwanza jamaa
huyo mwenye utajiri wa kutupwa alianza kwa
kuelezea namna alivyoshtuka aliposikia Zari ni
mjamzito.
ASHANGAA KUSIKIA ZARI MJAMZITO
Alisema kwamba alishangaa kusikia Zari ni
mjamzito wakati ana umri wa karibia miaka 40 na
watoto watatu ambao amekuwa akiwapuuza na
kuendelea kuzurura na mpenzi wake mpya,
Diamond sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bara la
Afrika.
Ivan Ssemwanga akiwa na 'Zari'
TATIZO UMRI?
Ilielezwa kwamba Ivan aliweka wazi kuwa
amekuwa na hofu kwa kuwa Zari ni mwanamke
ambaye umri umemtupa mkono hivyo anaweza
akashindwa na ‘stresi’ za malezi ya mtoto mchanga.
Maoni ya Ivan ameyatoa baada ya Diamond
kufichua kwamba Zari ni mjamzito huku akitupia
vielelezo vya vipimo mitandaoni vikionesha kiumbe
anayekua tumboni kwa mwanamke, jambo
lililosababisha jamii kuamini kuwa ni Zari kwa kuwa
wawili hao wamekuwa wakionekana kimahaba na
kulala chumba kimoja kwenye hoteli mbalimbali.
Jamaa huyo alisema yeye ameshazaa na Zari
watoto watatu na kwa pamoja walikubaliana
kwamba Zari asilete kiumbe mwingine duniani.
NI AJABU?
Kwa mujibu wa Ivan, aligundua kwamba Zari hawezi
kuwatunza vizuri watoto wake hivyo ni ajabu kuona
anaongeza mwingine.
“Kwa ninavyomjua Zari, naapa hawezi kuzaa na
Diamond,” alikaririwa jamaa huyo bila kufafanua
kama mimba ambayo tayari Zari anayo itakwenda
wapi
UMRI WA MWISHO KUZAA NI UPI?
Kutokana na maelezo ya Ivan, Ijumaa Wikienda
liliingia mzigo kutaka kujua umri wa mwisho wa
mwanamke kuzaa ni upi?
Kwa mujibu wa mtaalamu wetu, umri wa miaka 41
bado mwanamke ana uwezo wa kushika mimba
kama hana matatizo yoyote ya kiafya ambayo
yanaweza kuzuia kwa namna moja au nyingine
asishike mimba.
Mara nyingi muda hasa wa mwisho kabisa ni umri
wa miaka 45 endapo pia mwanamke anakuwa hana
tatizo la kiafya.
Hata hivyo, umri mzuri wa mwisho wa kuzaa kwa
mwanamke unaoshauriwa ni miaka 40 kwani
nyonga zinakuwa zimeanza kuchoka hasa kama
mama atakuwa amezaa kabla.
TURUDI KWA ZARI
Kwa maelezo ya mtaalam wetu, hata kama
mwanamama huyo anakaribia umri wa miaka 40 si
kigezo cha kushindwa kumzalia Diamond hivyo
kinachohitajika ni uangalizi wa hali ya juu.
Related Posts
MWANAMKE MMOJA AWAUWA WANAE NA KUWAZIKA NDANI
Hii Dunia sijui inaelekea wapi, na sijui mwisho wake ni nini... lakini nahisi nakosea kuilaumu Dunia[...]
Jan 26, 2015MSHINDI WA BIG BROTHER 2014 ANUNUA NYUMBA YAKIFAHALI
Ule usemi kuwa hakuna ‘baba/mama mwenye gari’ mjini bali kuna ‘baba/mama mwenye ny[...]
Jan 23, 2015WHY OBAMA'S INDIA REPUBLIC DAY VISIT IS SIGNIFICANT
The most significant aspect of the US President, Barack Obama's upcoming summit with the Indian Prim[...]
Jan 22, 2015MWANAUME MWENYE HIPS KUBWA KUWAZIDI KIM K,NICK MINAJ NA MASOGANGE
Micah ni mwanaume…lakini ana hips kama au zaidi ya mwanamke! Zile hips ambazo baadhi ya wadada[...]
Jan 20, 2015VANESSA MDEE KUTHIBITISHA KWA PICHA MAUSIANO YAKE NA JUX
Kwa mara kibao Vanessa Mdee na Jux wamekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi licha ya kuonesha dalil[...]
Jan 20, 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.