0

Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi
wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake
cha dini kinarushwa katika kituo kimoja
maarufu cha televisheni Bongo (Jina
tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la
Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata
aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya
kunaswa na mke wa mtu chumbani.
Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’
akijistili kwa kanga baada ya fumanizi
hilo.
Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya
jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu
Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu
waache dhambi alionekana akinyata kuingia
kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo
Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa,
mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi
wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za
Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake,
maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika
kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa
kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko
ndani, aliuliza namna ya kuwapata makamanda
wa Operesheni Fichua Maovu ya Global
Publishers ‘OFM’ ambapo mmoja wa majirani
alimpatia namba ya simu, akawapigia.
...Akivaa shati huku kitendea kazi chake
(Biblia) kikiwa nyuma yake.
Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo,
wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa
doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika
nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya
askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa
ushirikiano.
OFM watinga eneo la tukio
Baada ya makamanda wa OFM kupigiwa simu
na kunyetishiwa juu ya uwepo wa Muinjilisti
huyo chumbani na mke wa mtu, kwa kutumia
pikipiki zao ziendazo kasi walianza safari na
baada ya dakika chache walikuwa wamefika
kwenye nyumba hiyo na kuwakuta polisi.
Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi wakiwa na OFM waliongozwa na wifi mtu
huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi
yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta
mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu
wakiwa kama walivyozaliwa.
Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi
huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu
ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe
picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe
nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti
mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa
nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa
amefura ile mbaya.
Mchungaji huyo akijitetea baada ya
fumanizi hilo.
Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa
kujichanganya, awali alisema aliitwa na
mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo
ya biashara na kwamba eti walivua nguo
kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani
humo.
Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti
huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia
majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi
kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana
mume.
Bofya hapa usikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali
ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke
hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita
kwa ajili ya biashara flani.
“OFM nawajueni lakini niko chini ya miguu
yenu, naomba msiitoe habari hii gazetini kesho
n’tawaletea chochote pale ofisini kwenu, si ni
pale Bamaga ee, napajua sana pale”.
Mke wa mtu akijifunika kwa aibu.
OFM ni mwiko kupokea rushwa
Licha ya utetezi wake huo, makamanda wa OFM
walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza
kuwa, rushwa kwao ni mwiko hivyo kama
atafika ofisini kwao iwe ni kwa ajili ya maelezo
zaidi ya kwa nini amevunja moja ya amri kumi
za Mungu.
Mpaka OFM wanaondoka eneo la tukio, mke wa
mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba
msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye
akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai
kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua
ataaibika.
Ni fundi Blog hili limefikia hatua ya kuiandika habari
hii ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao
wamekuwa na tabia ya kuvuruga ndoa za watu
ikiwa ni pamoja na kufanya mambo mengine
ambayo ni kinyume na maadili.

Chapisha Maoni

 
Top