0

Warioba apigilia msumari escrow
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema pamoja na
kutoa
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba.PICHA|MAKTABA
ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
amesema pamoja na kutoa maazimio manane
kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni katika
Akaunti ya Tegeta Escrow, Bunge limefanya
makosa ya kutozijumuisha Wizara ya Fedha na
ile ya Viwanda na Biashara katika uchunguzi
huo kwa kuwa nazo zinahusika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini
kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alitaja
mambo manne aliyoyatilia shaka katika uamuzi
huo wa Bunge, akisema yalilenga kulindana.
Mambo hayo ni msingi wa hukumu kwa
watuhumiwa, wahusika wengine kutotajwa,
mwingiliano wa mamlaka ya mihimili ya dola na
wizara hizo kuachwa.
“Naona kama kulikuwa na namna fulani hivi ya
kulindana. Uamuzi wa Bunge ulifikiwa kutokana
na msukumo wa wananchi wa kutaka kujua
hatima ya suala la escrow na IPTL, wahisani
kusitisha msaada kwa sababu ya uchotwaji huo
wa fedha pamoja na siasa, hasa zinazolenga
urais mwaka 2015.”
Jaji Warioba alisema katika ripoti ya CAG na
PAC, wametaja ukiukwaji wa malipo ya kodi ya
ongezeko la mtaji (capital gain) na ushuru wa
stempu (stamp duty) na kuwa wanaohusika
katika hilo ni Wizara ya Fedha na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na upande mwingine ni
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela)
ambao uko chini ya Wizara ya Viwanda na
Biashara.
Alisema wanaotakiwa kuidhinisha ulipwaji wa
kodi ni TRA, huku akihoji kitendo cha ripoti
hizo mbili kuonyesha hisa zimeuzwa kwa Sh6
milioni wakati ilikuwa ni Dola 6 milioni,
nyingine kuuzwa kwa Dola 300,000 za Marekani
wakati ilikuwa Sh20 milioni.
“Hapa kuna ufisadi, maana hata kampuni
iliyotajwa kuwa imesajiliwa Brela inaonyesha
katika ripoti kuwa wahusika walioisajili
hawakuweka majina yao, waliweka saini tu,”
alisema.
Alisema uamuzi wa Bunge uliilenga Wizara ya
Nishati na Madini lakini hasara iliyotajwa
kuonekana inazihusu zaidi Wizara ya Fedha na
ile ya Viwanda.
“Kulikuwa na mchezo wa siasa, kwamba baadhi
walindwe na wengine waachwe. Taarifa ya
kamati imesema Kampuni ya PAP kwa
kushirikiana na ofisa wa ngazi za chini wa TRA
walidanganya. Hivi suala la kudanganya
linafanywa na maofisa wa chini tu, kwani wa
juu hawahusiki?”
Alisema kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kutakiwa kujiuzulu kwa maelezo
kuwa alikuwa akifahamu mlolongo wa wizi huo,
hata Hazina ilitakiwa kubanwa kwa sababu
nayo ilikuwa ikifahamu suala hilo...
“Tumeambiwa kuna uchunguzi unafanyika.
Jambo hili bado halijafikia mwisho, iweje
wengine waachwe wakati imeonekana wazi
kuwa Serikali imepata hasara?”
ADVERTISEMENT
Waliopata mgawo
Jaji Warioba alisema suala jingine lililokosa
majibu ni kitendo cha watu wanaodaiwa
kupewa fedha na James Rugemalira kutajwa
majina yao sambamba na akaunti ya aliyewapa,
lakini wale waliodaiwa kuchota fedha hizo
katika magunia hawakutajwa.
“Taarifa inasema waliolipwa fedha kupitia Benki
ya Stanbic walichukua fedha kwenye magunia
na mfuko, sasa mbona hawajatajwa? Hata
ukichukua fedha katika gunia lazima benki
itabaki na kumbukumbu ya jina la aliyechukua.
Tusubiri uchunguzi zaidi, ila naona kama ni
dalili za kulindana.
Msingi wa uamuzi
“Ili Bunge lipate msingi wa kufanya uamuzi huo
walisema fedha za escrow ni za umma na
wananchi wanaelewa fedha hizo ni za umma.
Binafsi nadhani katika hili Bunge halikutenda
haki,” alisema.
Alisema Akaunti ya Tegeta Escrow ilianzishwa
kwa sababu ya mvutano kati ya Tanesco na IPTL
ili kuweka fedha mpaka hapo mzozo huo
utakapomalizika... “IPTL imeendelea kutoa
huduma na umma umepata umeme kutoka
katika kampuni hiyo na kulikuwa na malipo.
Sasa kuja kumaliza tatizo lazima fedha za
escrow ndiyo zingetumika kulipia gharama zote
katika kipindi kile ambacho walikuwa
hawajakubaliana.
“Kwa maana hiyo huwezi kusema fedha hizo ni
za umma. Zilikuwa ni za kumlipa anayetoa
huduma ambaye ni IPTL, sasa kwa kuwa
hawakukubaliana juu ya gharama, waliamua
fedha zibaki mpaka tutakapokubaliana.
“Kama fedha hizo zingekuwa za umma
zingewekwa katika akaunti ya escrow kwa
misingi ipi? Tusubiri uchunguzi zaidi ili tujue za
umma zilikuwa kiasi gani na za watu binafsi
zilikuwa kiasi gani.”
Alisema kama kulikuwa na fedha za Serikali ni
kodi ambayo haikuwekwa wazi.
“Hii ambayo wameeleza kwamba Serikali
imepoteza Sh8 bilioni, ni kodi inayotokana na
mauzo ya hisa, siyo gharama za uwekezaji.
Ukiuza hisa lazima ulipe kodi ya ongezeko la
mtaji na ushuru wa stempu. Hiyo ndiyo hasara
wanayoisema na haihusiani na escrow kwa
sababu hata kama escrow isingekuwa na
matatizo, ilikuwa lazima walipe na ni utaratibu
wa kawaida,” alisema.

Chapisha Maoni

 
Top