Rappers/waimbaji 10 wa Bongo
wenye mbwembe (swag)
waongeapo redioni/TV
by kamandotz
Uongeaji ni sanaa pia ambapo kuna wale
waliojaaliwa uwezo wa kuongea kwa mbwembwe
zaidi na kuwa kivutio kwa wanaosikiliza. Hawa ni
wasanii 10 tunaoamini kuwa huongea kwa
mbwembwe zaidi wahojiwapo redioni ama kwenye
TV.
1. Godzilla
Kama haumfahamu Godzilla aka Zizi na hujawahi
kumsikia popote, ukifungulia redio na ukakuta
anahojiwa unaweza kuhisi ni mnyamwezi fulani
aliyekaa Marekani kwa muda mrefu sana na
Kiswahili kimeanza kumtoka kichwani. Tangu aanze
muziki, Zilla amekuwa akifuata nyendo nyingi za 50
Cent hasa katika kurap na kuongea. Mara nyingi
kwenye interview hutupia swag kama za 50 na kwa
hakika hakuna anayemfikia.
2. TID
Khalid Mohamed aka Top in Dar huongea kwa
kujiamini na dharau kiasi ndani yake (ndivyo alivyo).
Katika interview hupenda kuchanganya Kiingereza
mara kwa mara ambacho anakimudu poa pia.
Mfano mzuri ni kwenye U Heard ya jana ya XXL,
Clouds FM kuhusiana na kukwaruzana kwake na
Salama Jabir. Mwishoni mtangazaji wa show hiyo
Soudy Brown alimuuliza TID anafanya nini maskani,
na TID kujibu, “Nipo naangalia tambala moja hivi
kwenye 3D kwahiyo I need a lot of attention, I am
very sorry can you hang up for me!!”
3. Mr Blue
Blue amepunguza tu mbwembwe siku hizi lakini
kama ingekuwa enzi zile, Godzilla asingefua dafu.
Blue ni tozi kitambo na ndiye mhasisi wa utamkaji
wa maneno ya Kiswahili kwa ladha ya kimombo
kwa mfano kabisa itamkwe, kabaisa kitu
kilichofanya kuzaliwa kwa aka yake Kabayser.
4. Fid Q
Fid aka Ngosha si mkali tu wa mashairi yenye
swagga za moto bali pia hata uongeaji wake.
Pamoja na kwamba anatokea Mwanza ambako
Kiswahili cha huko kimeathiriwa na kisukuma, Fid
huongea kama kashuka jana kutoka states.
Uongeaji wake akiwa redioni utadhani ana
kigugumizi fulani kumbe ndio swag ziko on.
Izingatiwe pia kuwa The Top of Rap’s elite ni
profesa wa Kitaalojia.
5. P-Funk
Majani ni muongoezaji mzuri sana redioni.
Background yake ya elimu na kutembea sehemu
kadhaa duniani, kumemfanya asound kama
Mmarekani aongeapo kimombo.
6. Shetta
Shetta aka Bonge la Bwana naye yumo. Anapokuwa
akiongea redioni huwa haoni hatari kutupia maneno
kadhaa ya kimombo kushtua kidogo.
7. Q Chilla
Chilla ana uongeaji wa taratibu lakini wenye
mbwembwe za hapa na pale hasa za kuchomekea
viingereza.
8. Izzo B
Uvaaji wa Izzo na uongeaji wake vinaenda sawa.
Izzo ni bling blinger na hewani anapokuwa
anahojiwa, hit-maker huyo wa Riz-one hutupia
swagga kibao na kama anahojiwa na mtangazaji
mbovu si ajabu yeye ndio akasound kama
mtangazaji wa show, ana vocal kali.
9. Quick Rocka
Quick aka Switcher kama anavyojiita, ni rapper
anayeswitch swag kama kinyonga anavyobadili
rangi yake. Kama Izzo B, yeye pia ana sauti ya
mamlaka hewani.
10. Mo Rocka
Sijui nini kilitokea kwa rapper huyu mtanashati lakini
kwa speed aliyokuja nayo kama angekaza,
angekuwa mbali. Wakati anaanza kupata umaarufu
wengi walikuwa wakimfananisha na Kabayser hasa
kwa jinsi anavyorap na hata uongeaji wake kwenye
redio.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni